Mahakama ya mwanzo ya Pristina imempata na hatia Dusko Arsic kwa hatua yake ya kuwalazimisha raia kuondoka Pristina na katika maeneo ya kandokando yake kati ya Januari na Juni mwaka 1999.
Kulingana na uamuzi huo, Dusko Arsic pamoja na polisi kadhaa wa Serbia na vikundi vya wanamgambo walipora na kuharibu mali za raia wa Albania.
Arsic alitiwa mbaroni mwezi Disemba mwaka jana na alishtakiwa kwa kuhusika katika mauaji, udhalilishaji wa kingono na kisaikolojia wa raia wa Albania katika kijiji cha Butovic huko Pristina.
Wakili anayemtetea Arsic amesema atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
342/