Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Februari 2024

18:21:06
1435181

Abdollahian akosoa vikali mashambulio ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hujuma na mashambulio ya hivi karibuni ya Marekani katika mataifa ya Syria na Iraq chimbuko lake ni utendaji wa kimakosa na usio sahihi wa Washington katika kutatua matatizo ya Asia Magharibi kwa ktumia mtutu wa bunduki.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Hans Grunberg mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen na kusisitiza kuwa, hujuma na mashambulio ya kijeshi ya Marekani na Uingereza dhiodi ya Yemen na kuiweka Harakati ya Ansarullah ya Yemen katika orodha ya Washington ya makundi ya kigaidi ni mambo ambayo yatazidi kuifanya hali ya mambo kuwa tata zaidi.

Abdollahian ameashiria kuendelea himaya na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu katika kurejesha amani na usalama wa kudumu nchini Yemen na kueleza kwamba, hima na juhudi za kurejesha amani na uthabiti katikak eneo ni maslahi ya mataifa yote ya eneo hili. 

Kabla ya hapo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kana'an alisema Jumamosi kwamba."Shambulio la usiku (wa kuamkia Jumamosi) dhidi ya Syria na Iraq ni kitendo cha kichokozi na kosa jingine la kimkakati la serikali ya Marekani, ambalo halitakuwa na matokeo yoyote isipokuwa kuongezeka kwa hali ya wasiwasi na ukosefu wa utulivu katika eneo."

Watu 16 waliuawa, miongoni mwao wakiwa raia, na 25 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya usiku ya Marekani kwenye maeneo kadhaa Iraq, ofisi ya Waziri Mkuu Mohammed Shia' al-Sudani ilisema.

Mashambulizi ya Marekani mashariki mwa Syria na miji ya Al-Mayadeen na Al-Bukamal pia yamesababisha vifo vya watu 10 na kujeruhi wengine 18.

342/