Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

5 Februari 2024

19:13:58
1435508

Borrell: Mashambulizi ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq yanaweza kuzidisha mvutano

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell ameeleza wasiwasi wake kuhusu athari mbaya za mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq kwa hali inayogubikwa na wasiwasi ya eneo la Asia Magharibi, na kuonya kwamba hatua hizo zinaweza kuzidisha mivutano na kupanua wigo wa migogoro.

Akizungumza mwishoni mwa mkutano usio rasmi wa Mwaziri wa Mambo ya Jje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Josep Borrell ameashiria mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq, na kusema kwamba shambulio lolote litasababisha kuongezeka kwa mivutano, na mawaziri wa nchi za Ulaya walieleza wasiwasi wao kuhusiana na suala hilo katika mkutano wa Jumamosi iliyopita mjini Brussels.

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ameongeza kuwa, cheche yoyote inaweza kusababisha ajali kubwa zaidi, na kusema: "Tutajaribu kuzuia mkondo unaoshika kasi wa mashambulizi hayo." 

Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen pia imetoa taarifa ikilaani mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq, na kutangaza kuwa hatua za kichokozi za Marekani zitalitumbukiza eneo la Magharibi mwa Asia katika mzozo mkubwa zaidi na kutishia amani na usalama wa kimataifa.

Wakati huo huo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hossein Amir Abdollahian, amesema kuwa, hujuma na mashambulio ya hivi karibuni ya Marekani katika mataifa ya Syria na Iraq chimbuko lake ni utendaji wa kimakosa na usio sahihi wa Washington katika kutatua matatizo ya Asia Magharibi kwa kutumia mtutu wa bunduki.Kabla ya hapo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kana'an alisema Jumamosi iliyyopita kwamba: "Shambulio la Marekani usiku wa kuamkia Jumamosi dhidi ya Syria na Iraq ni kitendo cha kichokozi na kosa jingine la kimkakati la serikali ya Washington, ambalo matokeo yake ni kuzidisha hali ya wasiwasi na ukosefu wa utulivu katika eneo la Magharibi mwa Asia."

342/