Gazeti la The Guardian limebainisha katika ripoti yake ya Jumapili ya jana kwamba waandishi wa habari wa CNN huko Marekani na nje ya nchi hiyo wamelalamika waziwazi kuhusu kupotoshwa matangazo yanayohusu vita vya utawala wa Kizayuni wa Isarel dhidi ya watu wa Gaza kutokana na maagizo ya viongozi na wasimamizi wa televisheni hiyo.
Mfanyakazi mmoja wa televisheni ya CNN ameeleza bayana kuwa: Habari nyingi zimepotoshwa na televisheni ya CNN tangu Israel ianzishe vita Ukanda wa Gaza bila kuzingatia usahihi wa taarifa za awali kutokana na upendeleo wa kimfumo na kitaasisi ndani ya chombo hicho cha habari mkabala wa Israel. Amesema: "Urushaji matangazo unaofanywa na CNN kuhusu vita vya Israel huko Gaza ni kinyume na misingi ya uandishi wa habari." Gazeti la The Guardian limenukuu akaunti za mitandao ya kijamii za wafanyakazi sita wa televisheni ya CNN na zaidi ya kumbukumbu kumi na mbili za ndani pamoja na barua pepe kadhaa ilizopata na kuripoti kuwa: Makao makuu ya CNN huko Atlanta yameainisha miongozi mikali kuhusu namna ya kutangaza habari zinazohusiana na vita vya utawala wa Kizayuni wa Iisrael dhidi ya Ukanda wa Gaza ikiwa ni pamoja na hatua kali juu ya namna ya kuinukuu harakati ya Hamas na kutangaza taarifa nyingine kuhusu Palestina. Ripoti hiyo hiyo imeongeza kuwa kila habari kuhusu vita vya Gaza ni lazima itolewe maelezo na kufafanuliwa na ofisi ya CNN huko Jerusalem abla ya kutangazwa au kuchapishwa. Haya yote yanashuhudiwa wakati Mhariri Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CNN, Mark Thompson, ambaye alichukua uongozi siku mbili baada ya kuanza vita vya Israel dhidi ya Gaza, akituhumiwa kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya utawala wa Israel mara kadhaa alipokuwa mkurugenzi mkuu wa BBC miongo miwili iliyopita. Ripoti ya The Guardian imeendelea kuweza wazi kuwa: Upendeleo wa CNN kwa Israel umesababisha mgawanyiko ndani ya chombo hicho cha habari na hivyo kutoa mkusukumo kwa baadhi ya wafanyakazi kufikiria kuacha kazi.
342/