Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Februari 2024

15:22:55
1435777

Uhispania kuipatia UNRWA msaada wa dharura wa dola milioni 3.8

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania alitangaza jana Jumatatu kwamba nchi yake itatuma euro milioni 3.5 sawa na dola za Kimarekani milioni 3.8 kama msaada wa dharura kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA).

Hatua hiyo imekuja baada ya nchi kadhaa za Magharibu kusitisha ufadhili kwa UNRWA kufuatia madai ya Israel kuwa wafanyakazi kdhaa wa shirika hilo walihusika katika shambulio la Oktoba 7 la Hamas dhidi ya Israel kwa jina la Kimbunga cha Al Aqsa. Jose Manuel Albares Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania amesema kuwa msaada wa ziada utakusanywa ili kusaidia shughuli za shirika la UNRWA katika muda mfupi. Amesema, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) linatoa misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina milioni sita waliopo Jordan, Syria, Lebanon, Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania ameeleza kuwa, wakimbizi milioni 1.2 wanaoishi Ukanda wa Gaza wanategemea pakubwa misaada inayotolewa na shirika hilo ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Ameongeza kuwa, UNRWA imekataa tamaa na kuna "hatari kubwa" kwamba juhudi zake za kibinadamu huko Gaza zitasimama katika wiki zijazo. Amesema, "hali ya kibinadamu huko Palestina ni kipaumbele kwa ushirikiano wetu wa kimataifa."

342/