Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Februari 2024

15:25:32
1435781

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la kutolewa pigo kali la mataifa ya Kiislamu dhidi ya Israel

Kiongozi Muadhamu ametahadharisha kuhusu "maafa ya binadamu" yanayotokea Ukanda wa Gaza kwa himaya na misaada ya Marekani kwa utawala wa Israel na kubainisha kwamba, shakhsia na watu mashuhuri katika uulimwengu wa Kiislamu wanapaswa kuhimiza mwito wa kutoa pigo kali kwa utawala haramu wa Israel.

Ayatullah Seyyid Ali Khamenei alisema hayo Jumatatu ya jana katika mkutano wake na makamanda na wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Iran mjini Tehran kilichofanyika sambamba na maadhimisho ya Alfajiri Kumi na kukaribia kumbukumbu ya bai na kiapo cha utii cha kihistoria cha askari wa anga kwa Imamu Khomeini (MA).

Nukta ya kwanza aliyoiashiria Kiongozi Muadhamu katika hotuba yake hiyo ni vita vya Gaza na maafa ya kibinadamu katika Ukanda huo. Takwimu za karibuni kabisa za Wizara ya Afya ya Palestina zinaonyesha kuwa, Wapalestina karibu 28,000 wameuawa shahidi na wengine takribani 67,000 wamejeruhiwa huku wengine wapatao 7,000 hawajulikani walipo ambapo inasadikiwa kuwa wamefunikwa na vifusi. Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, kwa akali Wapalestina 225 huawa shahidi kila uchao huko Gaza kwa mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel. Kwa hakika hii ni misdaqi na kielelezo cha wazi kabisa cha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala haramu wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza.

Licha ya jinai hizi za kutisha, lakini hadi sasa mataifa ya Kiislamu hayajachukua hatua ya maana ya kukomesha jiinai hizo za Israel. Misimamo hii dhaifu inatathminiwa na weledi wa mambo kuwa imechangia kuendelea kufanyika mauaji ya kizazi huko Gaza. Katika kivuli cha ukimya na kigugumizi cha tawala za Kiislamu kuhusiana na vita hivyo, katika hotuba yake ya jana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka wananchi wa mataifa ya Kiislamu kuweka mashinikizo kwa serikali zao kwa ajili ya kutoa pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni. Kwa hakika, mtazamo huu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran unabainisha ukosoaji wake dhidi ya utendaji wa serikali za Kiislamu katika kukabiiliana na jinai zinazofanywa na Israel huko Gaza.

Ayatullah Khamenei ameeleza bayana kuwa, wananchi wana uwezo wa kuzishinikiza serikali za nchi zao kukomesha himaya na uungaji mkono wao kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na hivyo kutoa piko kali na la mwisho.

Amesisitiza kuwa: "Pigo la mwisho halimaanishi kwenda vitani na utawala wa Kizayuni (Israel), lakini lina maana ya kukata uhusiano wa kiuchumi na utawala huo." Amesema: Ingawa utawala huu katili na wenye sifa za mbwa mwitu umechukua maisha ya wanawake, watoto na wagonjwa na kuua zaidi ya watu 20,000, baadhi ya nchi za Kiislamu bado zinaupatia misaada ya kiuchumi na kuna taarifa kwamba, hata zinausaidia kwa silaha.

Hadi sasa wananchi wa mataifa ya Kiislamu wamefanya maandamano mara chungu nzima wakitaka kusitishwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na pia uungaji mkono wa nchi za Kiislamu kwa watu wa Gaza. Maandamano ya mamilioni ya watu wa Yemen, ambayo yamefanyika mara nyingi katika miezi 4 iliyopita, ni moja ya hatua hizi.Hata hivyo maandamano hayo hayajaleta pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni wala kuuwekea mashinikizo utawala huo ghasibu wa kukomesha jinai zake dhidi ya Gaza. Katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa pigo hilo la mwisho lina maana ya "kukata uhusiano wa kiuchumi" kati ya nchi za Kiislamu na utawala wa Kizayuni. Wakati wa vita vya Gaza, utawala dhalimu wa Israel umeonyesha kwamba, mshipa wake wa uhai ni masuala ya kiuchumi na kwa kuwa vita hivyo vina gharama kubwa, hapana shaka kkuuwa, kukata uhusiano wa kiuchumi nchi za Kiislamu na Israel mbali na kutoa pigo kwa utawala huo, kunaweza pia kusababisha mashinikizo kwa wakazi wa Palestina inayokkaliwa kwa mabavu (Israel) na matokeo yake yatakuwa ni kushadidi maandamano ya wananchi ya kutaka kuhitimishwa vita dhidi ya Gaza.

342/