Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Februari 2024

12:42:11
1436185

Makampuni makubwa duniani yakata uhusiano wa kijeshi na Israel kufuatia mauaji ya kimbari Gaza

Makampuni makubwa duniani kote yameanza kukata uhusiano na utawala haramu wa Israel baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi uliopita kwamba mauaji ya yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza ni sawa na mauaji ya kimbari.

Itochu ya Japan, ambayo inashika nafasi ya 96 kwenye orodha ya Fortune Global 500 ya makampuni makubwa zaidi duniani, ilitangaza kuwa shirika lake la usafiri wa anga linamaliza mkataba wake na shirika la  Elbit, mkandarasi mkuu wa kijeshi wa utawala wa Israel.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Itochu, Tsuyoshi Hachimura, alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari kwamba, kwa kuzingatia agizo la Mahakama ya Kimataifa ya Haki mnamo Januari 26, na kwamba serikali ya Japan inaunga mkono jukumu la mahakama hii, tayari tumesimamisha shughuli mpya zinazohusiana na mapatano yetu na Elbit."

Katika hatua sawa na hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Albares alitangaza siku ya Jumanne kwamba Madrid ilisimamisha mauzo yote ya silaha kwa utawala haramu wa Israeli tangu kuanza kwa vita vya Israeli dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Uhispania ametaja jinsi wanajeshi katili wa utawala ghasibu wa Israel walivyoshambulia kwa mabomu vituo, shule na hospitali za Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Albares aidha amebainisha kuwa, wanajeshi katili wa Kizayuni tayari wamewaua kwa umati zaidi ya Wapalestina 27,000 katika mashambulizi ya kikatili, ulipuaji wa mabomu na makombora huko Ghaza katika kipindi cha miezi minne iliyopita.