Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Februari 2024

12:45:40
1436190

Msomi Mnigeria: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni dhihirisho la kupigania uhuru duniani

Mwanasiasa na mwandishi mashuhuri wa Nigeria amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyoongozwa na Imam Khomeini (RA) ni kigezo cha wapigania uhuru kote duniani ili kuzifanya nchi zao kuwa huru.

Muhammad Ibrahim Gamawa amesema hayo kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Iran Press huko Abuja Nigeria na kueleza kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa Imam Khomeini (RA) yaliwasha taa ya uhuru duniani na mapinduzi haya ya watu yamekuwa nembo ya uhuru duniani.

Msomi huyo wa Kinigeria ameeleza kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamewafundisha watu huru duniani jinsi ya kuzikomboa nchi zao kutoka kwa utawala wa wakoloni na vibaraka wao.

Kuhusiana na kubakia na kudumu kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran licha ya vikwazo na njama za ubeberu wa kimataifa, Muhammad Ibrahim Gamawa amesisitiza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran pamoja na watu wake wenye nguvu yamesimama kwa miongo kadhaa bila ya kutetereka na kukwamisha njama zote za mabeberu.

Aidha mwanafikra huyo wa Nigeria amesema kuwa Imam Khomeini (RA) aliweka misingi imara ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kwamba, haiwezekani kuyasambaratisha mapiinduzi haya. Kadhalika amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ya wananchi wa Iran yamepata waungaji mkono katika sehemu mbalimbali za dunia na kila mtu ana ndoto ya kuwa na nchi kama Iran, kwa sababu Mapinduzi ya Kiislamu hayajatwishwa kwa mtu yeyote.


342/