Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Februari 2024

12:46:22
1436192

Mafanikio ya Iran katika siasa za ndani za kipindi cha miaka 45 iliyopita

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa katika siasa zake za ndani na nje kwenye kipindi cha miaka 45 ya Mapinduzi ya Kiislamu humu nchini.

Moja ya mafaniklio muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika siasa za  ndani ni uendeshaji wa mfumo wa utawala wa demokrasia ya kidini. Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran ilitawaliwa na mfumo wa kifalme ambao msingi wake ni tawala za kiukoo za kurithishana watu wa ukoo mmoja tu, lakini baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuliasisiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran ambao msingi wake mkuu ni kutegemea rai za wananchi na kufuata na kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu. 

Uhuru wa mihimili mitatu ya dola ambayo ni  Serikali, Bunge na Mahakama ambayo ndizo nguzo za mifumo ya kidemokrasia na kufanyika zaidi ya chaguzi 40 daima na kwa utaratibu maalumu, uhuru katika uchukuaji maamuzi na utekelezaji wa maamuzi hayo katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, pamoja na kuwajibika viongozi wa nchi na serikali mbele ya wananchi, ustawi wa sekta binafsi na vyama vya Kisiasa na... yote hayo ni katika mambo yanayotia nguvu mfumo wa demokrasia katika jamii ya leo ya Iran ya Kiislamu.

Jamhuri ya Kiislamu imeweza kuleta uwiano katika mambo mawili makuu, dini na siasa na kuanzisha  mfumo wa utawala wa kidini na kisiasa ambao umejengeka juu ya misingi wa utawala wa maadili ya Kiislamu na muundo wa demokrasia ya wananchi. Mfumo huo wa kiutawala ni wa Jamhuri unaozingatia sana maamuzi ya wananchi ni mfumo pia unaotegemea na kuyapa umuhimu mkubwa maadili na mafundisho ya Uislamu na kuifanya dini ya Kiislamu kuwa ndiyo marejeo makuu ya mfumo huo wa kiutawala. 

Kimsingi ni kwamba maamuzi ya wananchi na Uislamu ndizo nguzo mbili kuu za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vitu hivyo viwili viko pamoja muda wote na havitengani bali kila kimoja kinakitegemea kingine. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongiozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema: Nguzo mbili hizo yaani maamuzi ya wananchi na kuzingatia mafundisho ya Uislamu yanategemea uchaguzi, kwa sababu utawala wa wananchi katika nchi hauwezi kuimarishwa bila ya kuwepo chaguzi katika nchi hiyo za kuulizwa wananchi maoni na rai zao.

Ustawi wa kisiasa ni mafanikio mengine muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha miaka 45 iliyopita. Moja ya mafanikio muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ni uhuru wake wa kisiasa. Hii ni katika hali ambayo utawala wa taghuti yaani wa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, haukuwa na uhuru kwa kiwango chochote kile. Lakini Jamhuri ya Kiislamu sambamba na kupinga udhibiti wa madola ajinabi na badala yake kuliletea taifa la Iran nguvu za kuajiamulia lenyewe mambo yake, ilivuruga pia mipango haramu ya madola ya kibeberu inayokwenda kinyume cha utaratibu wa kimataifa. Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu una uhuru wa juu zaidi pia, ukilinganisha na nchi za eneo na nchi nyingi za dunia. Sera ya "Si Mashariki wala ya Magharibi" iliigeuza Iran ya Kiislamu, ambayo ilikuwa chini ya ushawishi wa madola ya kikoloni na ya kigeni katika zama hizo, kuwa nchi isiyoweza kudhibitika na huru kabisa.