Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Februari 2024

12:46:56
1436193

Eslami: Iran imejitosheleza katika sekta ya nyuklia

Mohammad Eslami Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema, leo hii sekta ya nyuklia ya Iran hususan katika uga wa mzunguko wa mafuta ya nyuklia imejitosheleza na sasa inategemea wataalamu wa ndani ya nchi kikamilifu.

Kwa mujibu wa IRNA; Mohammad Eslami aliyasema hayo katika hafla ya kuzindua kifaa cha  cha spectrometa ya sumaku kilichopewa jina la Iranium katika Jumba la Uturubishaji la Shahid Ahmadi Roshan huko Natanz. Amesema lengo la adui tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilikuwa ni kuweka mipaka na kuzuia ustawi wa nchi katika nyanja mpya ambazo ni udhihirisho wa uwezo na kujiamini.

Ameongeza kuwa: "Msingi na lengo kuu la Mapinduzi ya Kiislamu lilikuwa ni kupata kujiamini na imani ya kimaendeleo kwa kuegemea imani za kitaifa na kidini, jambo ambalo maadui hawakulitafakari."Islami alisema: Waliweka vikwazo vya pande zote dhidi ya tasnia ya nyuklia ya nchi Iran na pia walitekeleza njama za uharibifu wa viwanda , na ugaidi kwenye ajenda zao na walijaribu kuzuia shughuli zetu kwa kuvuruga michakato ya sasa.

Ameendelea kufafanua kuwa: "Leo hii sekta ya nyuklia ya Iran imepata nafasi nzuri hususan katika uga wa mzunguko wa uzalishaji fueli ya nyiklia. Hii inahesabiwa kuwa teknolojia muhimu zaidi katika uga wa kimataifa na yenye matumizi mengi tofauti, na Iran hivi sasa inajitosheleza katika masuala mbalimbali. 

Eslami amesema chombo kipya cha Iranium kilichoundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran  hutumika kupima wigo wa atomi ambazo zipo katika dutu na kuogeza kuwai matumizi yake ni mapana katika tasnia isyo ya nyuklia.


342/