Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Februari 2024

12:48:26
1436196

Kiongozi wa Kanisa Katoliki awaita 'wanafiki' wanaopinga uchafu wa LGBT

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amesema kuwa, anaona ni "unafiki" maneno ya wale wanaokosoa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki watu wenye makhusiano machafu ya jinsia moja maarufu kwa jina la LGBT.

Mwezi uliopita wa Januari, Kanisa Katoliki katika makao yake makuu ya Vatican lilibariki vitendo vichafu vya mahusiano haramu ya watu wa jinsia moja maarufu kwa jina la LGBT kwa kutumia hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust). Hatua hiyo imekumbwa na upinzani mkubwa hata ndani ya Kanisa Katoliki kwenyewe, hususan kutoka kwa maaskofu wa barani Afrika.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ameendelea kupotosha watu kwa kudai kuwa anapowabariki watu wanaofanya makosa mengine haiwi tatizo lakini anapowabariki watu wanaojihusisha na vitendo vichafu vya mahusiano ya jinsia moja kunapigwa makelele mengi. Ametoa madai hayo bila ya kujali athari mbaya na madhara makubwa ya kijamii ya kila kosa na kwamba makosa yana daraja tofauti.

Papa Francis pia amesema daima anawakaribisha kanisani watu wanaojihusisha na vitendo vichafu vya mahusiano ya jinsia moja akidai kuwa na wao ni viumbe wa Mungu hivyo wanakaribishwa kuungama makosa yao kanisani. Papa Francis ametoa madai hayo bila ya kujali kuwa watu hao LGBT hawakiri kuwa uchafu wanaofanya ni kosa na hawana nia yoyote ya kutubu, bali wanajifakharisha kwa uchafu huo na wanafanya kampeni kubwa ya kuwaingiza watu wengine kote ulimwenguni kwenye shimo la uchafu wao huo. 

Wafuasi mbalimbali wa Kanisa Katoli wanasema kuwa hatari ya uamuzi huo wa Papa ni pamoja na kudhoofisha mafundisho na maadili ya Kanisa. 

342/