Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

10 Februari 2024

14:26:29
1436647

Marekani mhusika wa kuendelea mauaji ya kimbari ya Wazayuni Ukanda wa Gaza

Himaya na uungaji mkono wa madola ya Magharibi hususan Marekani kwa utawala haramu wa Israel kivitendo umezuia kusitishwa vita na hilo kuandaa uwanja wa kuendelea kuuawa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Utawala wa Kizayuni umekuwa ukiungwa mkono na Wamagharibi katika vita vyote na nchi za Kiarabu na makundi ya muqawama ya Palestina na Lebanon, na hivi sasa pia unaendeleza vita vya Gaza kwa uungaji mkono kamili wa madola ya Magharibi.

Baada ya operesheni ya muqawama wa Palestina ya Kimbunga cha al-Aqswa tarehe 7 Oktoba mwaka jana (2023), utawala wa Kizayuni umefanya mashambulizi ya anga na ardhini yasiyo na mithili katika Ukanda wa Gaza. Karibu watu 30,000 wameuawa shahidi na takriban Wapalestina 68,000 wamejeruhiwa.

Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Katika kipindi hiki baadhi ya nchi ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeanzisha harakati kubwa kwa lengo la kusimamisha mauaji ya Wazayuni, lakini wahusika wakuu wa nchi za Magharibi kama vile Marekani, Uingereza na Ufaransa waliongeza njama za kuzuia kukomeshwa vita hivyo. Uungaji mkono wa kisiasa, kijeshi na kifedha na pia kuzuia kuidhinishwa Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kutaka kukomesha vita ni mambo ambayo yamesababisha mauaji ya kimbari ya Wazayuni kuendelea katika Ukanda wa Gaza.

Sambamba na kuanza vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, serikali ya Marekani ilishadidisha utumaji wa kila aina ya silaha, risasi na mabomu kwa utawala huo, na hata Rais wa Marekani Joe Biden katika siku za kwanza za vita hivyo akiwa na lengo la kuunga mkono jinai za Wazayuni huko Gaza, alisafiri hadi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kukutana na na kufanya mazungumzo na maafisa wa Tel-Aviv.

Hii ni katika hali ambayo, misaada ya kifedha ya Marekani pia huongezeka baada ya kila uingiliaji wa kijeshi na ukandamizaji wa Wapalestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni ambapo hatua ya karibuni kabisa ni kwamba, wiki ijayo Baraza la Wawakilishi la Marekani litapiga kura kuhusu mpango wa msaada wa dola bilioni 17.6 kwa utawala wa Kizayuni.

Kuendelea mchakato huo kunaonyesha kuwa, kama ambavyo kuasisiwa utawala bandia wa Kizayuni kulikuwa ni natija ya siasa za madola ya Magharibi katika eneo hili, kuendelezwa mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Palestina pia kunafanywa kwa uungaji mkono wa madola hayohayo, ikiwa ni pamoja na Marekani, na katika fremu ya malengo ya kibeberu. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitambulisha Marekani kuwa ni mshirika wa jinai za Wazayuni.

Akizungumza Alkhamisi ya juzi katika mkutano na viongozi na watendaji wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, mabalozi na wawakilishi wa nchi za Kiislamu pamoja na wananchi wa matabaka tofauti uliofanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha Idi ya Mab'ath ya kupewa Utume Nabii Muhammad Al Mustafa SAW, Ayatullha Sayyid Ali Khamenei, aliashiria tukio chungu na la kuhuzunisha la Gaza na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni, na akasema: “masaibu ya Gaza ni masaibu ya wanadamu na yanaonyesha kuwa utaratibu wa sasa wa ulimwengu ni wa batili tupu, usioweza kudumu na utatoweka tu.


342/