Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

10 Februari 2024

14:27:44
1436649

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso: Iran ni kigezo cha muqawama

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso ameshiriki katika sherehe za madhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kigezo bora cha utawala, muqawama, ushujaa na mapambano.

 Bi Stella El Din, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso amesema hayo mjini Ouagadougou na kuongeza kuwa, sisi tunaichukulia Iran kuwa ni kigezo ya utawala, muqawama na msimamo imara kwani tumepata funzo kutokana na ushujaa na kusimama kidete Iran katika kukabiliana na hali ngumu ambayo madola ya kibeberu yameibebesha Tehran.

Amesema hayo katika sherehe zilizohudhuriwa pia na Mujtaba Faqihi, Balozi wa Iran nchini Burkina Faso na kusisitiza kuwa, siri ya kubakia imara na kuwa na nguvu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi chote hiki cha miaka 45 ya mashinikizo na vikwazo vya kila namna ni kuwa kwake huru kisiasa na ni kutokana na mfumo wake wa utawala ambao unategemea wananchi wake na sheria za Kiislamu. Amesema: Mfumo wa utawala wa Iran ni wa kipekee na si wa kuiga kutoka nje ya nchi.

Sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu zinaendelea kufanyika katika kona mbalimbali duniani ikiwemo Moscow Russia ambapo Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu nchini humo, Kazem Jalali amesema katika sherehe hizo kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran yamepata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi. Amesema: Marekani inashindwa kuelewa vilivyo mabadiliko ya ukanda wa Asia Magharibi na inadhani kuwa mrengo wa muqawama unaishia tu kwenye eneo dogo la Ukanda wa Ghaza lakini makundi mengine ya muqawama katika eneo hili yameithibitishia kivitendo Marekani na utawala wa Kizayuni kwamba Ghaza haiko peke yake na hadi sasa makundi hayo yametoa somo zito na chungu kwa mabeberu Wazayuni.


342/