Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

10 Februari 2024

14:28:19
1436650

Iran yaonya kuhusu uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya vikali Marekani dhidi ya kuendelea kuiunga mkono Israel na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.

Hossein Amir-Abdollahian alitoa indhari hiyo jana Ijumaa baada ya kuwasili Beirut, mji mkuu wa Lebanon na kuongeza kuwa, ungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel hautakuwa na matokeo mengine ghairi ya kushindwa kukubwa.

Amir-Abdollahian amewaambia waandishi wa habari mjini Beirut kuwa, "Utawala wa Kizayuni (Israel) unataka kuigharikisha Marekani katika kinamasi cha vita katika eneo la Asia Magharibi."

Amesema utawala pandikizi wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake batili katika Ukanda wa Gaza kutokana na kusimama kidete makundi ya muqawama ya Palestina, Lebanon na eneo zima la magharibi mwa Asia.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amepongeza kwa njia ya kipekee Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwa kukabiliana kishujaa na Israel, huku akiwaenzi mashahidi wa makundi ya mapambano ya Palestina na Lebanon.Kabla ya hapo, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran alilaani vitendo vya uchokozi vya hivi karibuni dhidi ya nchi za Asia Magharibi na kuzionya Marekani na Uingereza kwamba, zisijaribu kuzipima ghadhabu za mataifa ya eneo hili.

"Iran itaendelea kuunga mkono muqawama na Lebanon. Tunatazama usalama wa Lebanon kuwa usalama wa Iran na usalama wa eneo zima (la Asia Magharibi)," ameongeza Amir-Abdollahian.


342/