Main Title

source : Parstoday
Jumapili

11 Februari 2024

19:16:48
1436864

Wairani wanashiriki maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mamilioni ya wananchi wa Iran wanashiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 kwa uongozi wa Imamu Ruhullah Khomeini (MA).

Maandamano hayo yanayoambatana na sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yanafanyika leo katika miji mbalimbali ya Iran.

Katika mji mkuu Tehran waandamanaji wameonekana wakiwa wamebeba mabango na maberamu ya kuilaani Marekani, Israel na washirika wao na jumbe nyingine zinazosisitiza kusimama kidete taiifa hili dhidi ya maadui wa mapinduzi haya.

Maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran yanatarajiwa kuishia katika Mzunguko wa Azadi ambapo Rais Ebrahim Rais anatarajiwa kuwahutubia waandamanaji. 

Ikumbukwe kuwa, miaka 45 iliyopita katika siku kama ya leo, Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote.

Siku hiyo wananchi waliokuwa wakipiga takbira na kutoa nara za kimapinduzi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung’oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu.

342/