Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

12 Februari 2024

19:26:14
1437182

22 Bahman mahudhurio ya hamasa ya Wairan na sisitizo la kusimama kidete

Jumapili ya jana, tarehe 22 Bahman (Februari 11) ilisadifiana na maadhimisho ya mwaka wa 45 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Mwaka huu, kama ilivyokuwa miaka iliyopita, wananchi wa Iran walikuwa na mahudhurio makubwa na ya hamasa katika maandamano ya Yaumullah 22 Bahman katika mikoa tofauti ya Iran.

Mahudhurio makubwa na mshikamano wa wananchi wa Iran katika maandamano ya 22 ya Bahman katika kipindi cha miaka 45 iliyopita yamegeuka na kuwa nembo ya kusimama kidete, umoja na sherehe za ushindi wa taifa la Iran dhidi ya mfumo wa kibeberu.

Siku hii ya kitaifa ni ukumbusho wa moja ya matukio makubwa ya kihistoria ya taifa la Iran; taifa ambalo limeingia mitaani katika kipindi cha miaka 45 katika hali yoyote ile na kuonyesha umoja na mshikamano wake kwa ulimwengu katika kulinda thamani za mapinduzi.

Katika miaka hii, mashambulizi ya mabomu ya adui wa Kibaath katika miaka minane ya vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran, mashinikizo ya kisiasa navikwazo vya kiuchumi ya Marekani na waitifaki wake ni mambo ambayo  hayakuweza katu kutia dosari azma na irada ya taifa la Iran la kuendeleza njia ya mapinduzi.

Ushiriki wa wananchi katika matembezi ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni uwanja wa mwamko na umakini wao, umoja wao na uelewa wao, na kutilia maanani hatima ya nchi na kutangaza kuchukizwa kwao na maadui wa nchi. Mfumo wa Kiislamu ambao umekuwa chimbuko la faraja kwa marafiki wa mfumo wa Kiislamu na kusambaratisha njama za maadui wa ndani na wa nje wa mapinduzi hayo.

342/