Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

12 Februari 2024

19:26:41
1437183

Viongozi wa dunia, maafisa wakuu waipongeza Iran kwa maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu

Viongozi kadhaa wa dunia na maafisa wakuu na wizara za mambo ya nje wanaendelea kuipongeza serikali na taifa la Iran kwa kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika jumbe mbili tofauti siku ya Jumapili, Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia na Mwanamfalme Mohammed bin Salman walitoa salamu za pongezi kwa Rais wa Iran, Ebrahim Raisi kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika jumbe zao, viongozi hao wa  Saudia waliitakia maendeleo na ustawi zaidi serikali na taifa la Iran.

Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan Ilham Aliyev naye ametuma salamu na kusema uhusiano mzuri na wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili utastawi zaidi.

Katika jumbe tofauti, Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Naibu Amiri Sheikh Abdullah bin Hamad bin Khalifa Al Thani na Waziri Mkuu Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani wamempongeza Rais Raisi kwa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ujumbe wa pongezi kwa mwenzake wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tajikistan Sirojiddin Muhriddin alisifu mafanikio makubwa ya Iran baada ya ushndi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Naye msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova alitoa salamu zake za pongezi kwa Wairani na kusema Russia na Iran ziko kwenye njia ya kuunda "utaratibu mpya wa dunia."

Katika chapisho kwenye akaunti yake ya X, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilichapisha picha ya Uwanja wa Azadi mjini Tehran na bendera za Iran na Pakistan ambapo juu ya picha hiyo Wizara hiyo ilitoa pongezi zake za dhati kwa watu na serikali ya Iran.

342/