Main Title

source : Parstoday
Jumanne

13 Februari 2024

15:35:19
1437478

Viongozi wa Muqawama: Vita vya Ghaza si vita vya mwisho na Wazayuni

Viongozi wa makundi mbalimbali ya muqawama wa Palestina wameonana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus Syria na kusisitiza kuwa, mapambano ya taifa la Palestina tangu Wazayuni walipovamia ardhi za taifa hilo zaidi ya miaka 75 iliyopita, vimekuwepo na vitaendelea hadi kila shibri ya ardhi ya Palestina itakapokombolewa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonana na karibu viongozi 15 wa makundi mbalimbali ya muqawama wa Palestina mjini Damascus Syria na kujadiliana nao masuala tofauti. 

Viongozi wa makundi ya mapambano ya Palestina walioshiriki kwenye mazungumzo hayo wameishukuru Jamhuri ya Kiislamu kwa uungaji mkono wake mkubwa wa taifa na kadhia ya Palestina na kuongeza kuwa, vita vya hivi sasa vya Ghaza havitokuwa vya mwisho dhidi ya utawala wa Kizayuni.

342/