Main Title

source : Parstoday
Jumanne

13 Februari 2024

15:35:44
1437479

Mapitio ya safari ya kieneo ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran

Sambamba na kuendelea kutokota mgogoro katika eneo la Asia Magharibi na kuendelea mauaji ya halaiki ya Wazayuni maghasibu huko Gaza Palestina, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya safari katika mataifa ya Lebanon na Syria.

Baada ya kuondoka Damascus Syria, Hussein Amir-Abdollahian amepanga kuelekea Qatar.

Ziara hii ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, imefanyika katikati ya kilele cha mzozo na mvutano wa vita huko Gaza, kwa sababu inaonekana kuwa utawala wa Kizayuni ambao haujapata matokeo uliyotakaa kutokana na kuendelea mauaji ya halaiki dhidi ya taifa la Palestina, sasa unafanya maafa mapya ya kibinadamu huko Rafah ukiwa unafuatilia kufidia kushindwa kwake kisiasa na kijeshi katika vita vya Gaza.

Katika hali hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikwenda Beirut ambako alikutana na kufanya mazungumzo Samahat Seyyid Hassan Nasrallah", Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, viongozi wa makundi ya muqawama na maafisa waandamizi wa serikali ya Lebanon. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisisitiza kuwa, adui Mzayuni yuko katika mgogoro wa kiistratijia na hajafikia malengo yake yoyote katika uwanja huo.

Katika mkutano huu, Amir Abdollahian alikumbusha kwamba, kukubalika kwa muqawama kama kambi kuu katika ubunifu wa kisiasa ni ishara ya nafasi kubwa na mchango ulionao muqawama wa Palestina na eneo hili kwa ujumla.

342/