Main Title

source : Parstoday
Jumanne

13 Februari 2024

15:36:22
1437482

Wasomi na wataalamu 3,700 wa Kiirani warejea nchini

Naibu Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mahusiano ya Kisayansi na Teknolojia anayehusika na Maendeleo ya Sayansi na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Rais wa Iran ametangaza habari ya kurejea nchini wasomi na wataalamu 3,700 wa Kiirani katika fremu ya mradi uliopewa jina la "Connect".

Wasomi ni mtaji wa watu wa nchi yoyote, ambao uwepo wao hupelekea kuwepo mlingano katika jamii, na ndio sababu kuu ya ustawi na maendeleo ya nchi husika. Jamii inapoishiwa wasomi suala hilo, licha ya kusimamisha mchakato wa maendeleo, huhatarisha pia utulivu wa jamii. 

Iran pia, sawa kabisa na aghalabu ya nchi zinazoendelea duniani, inakabiliwa na matatizo ya kukuza vipaji na  kubakisha nchini wafanyakazi waliobobea katika taaluma mbalimbali kutokana na kuwepo taasisi au watu wanaopigania maslahi yao na binafsi wanaowasaka wasomi na wataalamu wenye vipawa na kisha kuwahamishia katika nchi zilizoendelea. Mchakato wa uhamiaji wa wataalamu na wasomi wa Kiirani kwenda nchi zilizoendelea duniani umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Kuhusiana na suala hili, kitambo nyuma Sayyid Salman Sayyid Afqahi, Naibu Mkuu Taasisi ya Taifa ya Wasomi wa Iran, ameeleza kuwa taasisi hiyo inataka kuwasilisha na kuidhinisha muswada kwa ajili ya kuwasadia wasomi na kwamba muswada huo unatayarishwa katika tume husika ya bodi ya serikali na utawasilishwa katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge). 

342/