Main Title

source : Parstoday
Jumanne

13 Februari 2024

15:36:55
1437483

Iran: Kupanua jinai za vita dhidi ya Wapalestina wa Rafah kutakuwa na madhara makubwa kwa utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa onyo kali kwa mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuuvamia mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza na kusema kuwa utakuwa na madhara makubwa kwa utawala huo.

Hossein Amir-Abdollahian ameyasema hayo katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Kupanuka kwa jinai za kivita za utawala unaokalia ardhi kwa mabavu wa Israel na mauaji ya halaiki kuwajumuisha wakimbizi wa Kipalestina huko Rafah kutakuwa na madhara makubwa kwa Tel Aviv," umeeleza ujumbe huo. Amir-Abdollahian ametoa kauli hiyo baada ya mapema jana, Wapalestina wasiopungua 100, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kuuawa shahidi na wengine wapatao 230 kujeruhiwa katika mashambulizi makubwa ya anga na mizinga yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa Rafah. 

Wakati huohuo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kan'ani ametahadharisha kwamba hujuma za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Rafah na uvamizi wa ardhini katika mji huo zinaweza kusababisha "maafa mengine ya kibinadamu na jinai za kivita dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina."Kan'ani ameongeza kuwa uvamizi dhidi ya Rafah sio tu unakinzana na kuvuruga mazungumzo yanayoendelea kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano, lakini pia ni kinyume na uamuzi wa muda wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo iliiamuru Israel mwezi uliopita kuchukua hatua mara moja za kuzuia mauaji ya kimbari huko Gaza. Jeshi katili la utawala wa Kizayuni limefanya mashambulio hayo ya kinyama wakati zaidi ya watu milioni moja na laki nne, takriban mara tano ya idadi ya wakazi wa kawaida wa Rafah, wamekimbilia kwenye mji huo, huku utawala huo wa Kizayuni ukiendeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, ambayo tangu yalipoanza Oktoba 7, 2023 hadi sasa yameteketeza roho za Wapalestina zaidi ya 28,300. Siku ya Ijumaa, waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliamuru jeshi la utawala huo kujiandaa kuwahamisha raia kutoka Rafah kabla ya operesheni ya mashambulio ya ardhini iliyopangwa kutekelezwa dhidi ya mji huo. Mashirika ya misaada, hata hivyo yanasema, hatua kama hiyo ni sawa na jambo lisilowezekana, kwa kuzingatia ukubwa wa uharibifu uliosababishwa hadi sasa katika sehemu zingine za Gaza na idadi kubwa ya watu walionasa katika eneo hilo la Rafah lililozingirwa.../

342/