Main Title

source : Parstoday
Jumanne

13 Februari 2024

15:37:26
1437485

Iran yazindua kombora la balestiki la masafa marefu

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza habari ya kufanyia majaribio kwa mafanikio kombora la masafa marefu lililovurumishwa kutoka kwenye moja ya manowari za kivita za jeshi hilo la Iran.

Hayo yalitangazwa jana Jumatatu na Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa IRGC ambaye ameeleza kuwa, uzinduzi wa kombora hilo unamaanisha kuwa, SEPAH sasa ina uwezo wa kushambulia kwa usahihi shabaha yoyote ile, kwa kuwa meli zake za kijeshi zina uwezo wa kwenda popote pale duniani.

Kamanda Salami amebainisha kuwa: Kombora hilo la masafa marefu limezinduliwa katika shughuli ya pamoja ya Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Jeshi la Majini la IRGC.

Uzinduzi huo umefanyika mwezi mmoja baada ya IRGC kushambulia kwa makombora kadhaa ya balestiki, yakiwemo makombora 4 ya "Khaybar Shekan" ngome za makundi ya kigaidi hususan ISIS na majasusi wa Israel katika nchi za Iraq na Syria.

Jeshi la SEPAH lilisema shambulizi hilo lilifanyika kujibu jinai zilizofanywa hivi karibuni na makundi ya kigaidi katika miji ya Kerman na Rask, kusini mwa Iran.Mwishoni mwa mwaka uliopita pia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizindua kombora jipya la hypersonic lililopewa jina la 'Fattah 2' miezi michache baada kufanyiwa majaribio kombora jingine la hypersonic la 'Fattah'. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Iran, sekta ya viwanda vya wizara hiyo ina uwezo wa kuunda silaha za aina zozote zinazohitajika na vikosi vya ulinzi vya nchi hii. Mafanikio ya viwanda vya silaha vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan katika kuunda makombora ya balistiki katika miaka ya karibuni yameyatia tumbojoto madola ya Magharibi. 

342/