Main Title

source : Parstoday
Jumatano

14 Februari 2024

14:19:38
1437735

'Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu': Israel inawatesa na kuwanyanyasa mateka Wapalestina

Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini Geneva, limesema kwamba vikosi vya utawala haramu wa Israel vimewaruhusu walowezi wa Kizayuni kushuhudia mateso na udhalilishaji wa Wapalestina waliokuwa wakizuiliwa kutoka Ukanda wa Gaza wakati huu utawala huo unapoendeleza vita vya mauaji ya kimbari katika eneo hilo.

Kundi hilo la Euro-Med Human Rights Monitor limesema limepata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya wafungwa walioachiwa huru ambao walieleza kufanyiwa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji na udhalilishaji mbele ya walowezi hao.

Kundi hilo limesema unyanyasaji huo ulifanyika katika kambi ya kijeshi ya Zikim karibu na mpaka wa kaskazini wa Gaza na jela ya Negev kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ambapo wafungwa wengi walizuiliwa kwa wiki kadhaa bila kufunguliwa mashtaka.

Kwa mujibu wa mashuhuda, walowezi hao wa Kizayuni walifikishwa katika magereza mara kadhaa na kuruhusiwa kuwatazama, kuwapiga picha wafungwa hao ambao walilazimishwa kuvua nguo, kupigwa kwa fimbo za chuma na shoti za umeme, na kunyunyiziwa maji ya moto.

Mmoja wa wafungwa hao, Omar Abu Mudallala, 43, kutoka Gaza, aliiambia Euro-Med kwamba aliteswa na kunyanyaswa katika muda wote wa siku 52 alizokuwa kizuizini.

Euro-Med ilisema: "Jeshi la Israel kuwatesa na kuwatendea kinyama wafungwa wa Kipalestina ni kinyume cha sheria chini ya Mkataba wa Roma na ni uhalifu dhidi ya ubinadamu," na kuongeza kuwa unyanyasaji huu ambao ulikuwa kama burudani kwa walowezi wa Kizayuni "na upigaji picha wa

342/