Shirika la habari la FARS limemnukuu Mohammad Mokhber akisema hayo jana Jumanne kwenye kikao cha kupanga sera za maonyesho ya kimataifa ya IRAEXPO na huku akiashiria umaarufu na mapenzi waliyo nayo walimwengu wengi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu, Iran hivi sasa imepiga hatua kubwa za ustawi wa elimu, sayansi na teknolojia kwenye nyuga tofauti kama za uzalishaji wa bidhaa za viwandani, kilimo, teknolojia mpya na katika nyuga nyinginezo nyingi kiasi kwamba mara kwa mara maendeleo hayo ya Iran yamekuwa yakipongezwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran amesisitiza pia kuwa, msaada wa kutosha wa serikali ya Iran wa kuhakikisha maonyesho hayo yanafanyika kwa ufanisi mkubwa ni uthibitisho wa jinsi Serikali ya 13 wa Jamhuri ya Kiislamu inavyolipa umuhimu mkubwa suala la kutangazwa ipasavyo uwezo mkubwa ilio nao Iran katika uzalishaji wa bidhaa bora za kusafirishwa nje ya nchi. Maonyesho ya IRAEXPO 2024 ya kutangaza uwezo mkubwa wa Iran katika nyuga tofauti za uzalishaji bidhaa za kusafirishwa nje ya nchi, yanatarajiwa kufanyika kuanzisha tarehe 27 Aprili hadi tarehe Mosi Mei mwaka huu wa 2024 hapa jijini Tehran.
342/