Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

15 Februari 2024

14:22:08
1438019

Putin: Rais anayefaa zaidi Marekani ni Joe Biden si Trump

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa anafadhilisha Joe Biden aendelee kuwa rais wa Marekani kuliko kurejea madarakani Donald Trump.

Rais wa Russia amesema hayo pambizoni mwa kikao cha "Jumuiya ya Teknolojia za Mustakbali" mjini Moscow na kuongeza kuwa, yeye anaona ni bora Biden aendelee kuwa rais wa Marekani kwa sababu maamuzi yake yanatabirika lakini Doland Trump ni mtu wa kuchukua maamuzi yasiyotabirika.

Vile vile amesema, mbali na kwamba maamuzi ya Biden yanatabirika, lakini pia ana uzoefu na anafuata siasa za kizamani ingawa hapo hapo amesema kuwa, wenye uamuzi wa mwisho wa kuchagua nani awe rais wa Marekani ni wananchi wenyewe wa nchi hiyo.Siku chache zilizopita, Donald Trump ambaye anaomgoza katika kura za mchujo za chama cha Republican kwa ajili ya uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka huu wa 2024 alisema kuwa akiwa rais wa Marekani atahakikisha wanachama wa NATO wanatoa fedha nyingi kwa Washingto vinginevyo ataiachia Russia izifanye inavyotaka nchi za Ulaya wanachama wa NATO. Matamshi ya Vladimir Putin yamekuja siku chache baada ya matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika nchini Marekani kuonesha kuwa wananchi wengi wa nchi hiyo wanapinga Joe Biden kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais wa baadaye mwaka huu. Matokeo ya uchunguzi huo mpya uliofanywa na ABC na Taasisi ya Utafiti ya Ipsos yanaonesha kuwa, asilimia 86 ya Wamarekani wanaamini kuwa rais wa hivi sasa wa Marekani, Joe Biden, ni kizee mno na hana hadhi ya kuendelea kuweko kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Hayo yamekuja baada ya Robert Hoare, mchunguzi maalumu wa Idara ya Mahakama ya Marekani kutangaza kuwa, "Biden hata hakumbuki ni lini mtoto wake alikufa au zama alipokuwa makamu wa rais wa Obama."

342/