Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

24 Februari 2024

14:30:42
1440082

Iran yakanusha kuiuzuia makombora ya balestiki Russia

Ofisi ya mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha vikali madai ya baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vilivyodai kuwa, Iran imeiuzia Russia makombora ya balestiki ya kuyatumia kwenye vita vyake vya Ukraine.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, ofisi ya mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imesema kuwa, ingawa hakuna kizuizi chochote cha kisheria kinachoizuia Iran kuiuzia Russia makombora ya balestiki, lakini Tehran inachunga maadili na msimamo wake wa kuhakikisha kuwa vita vya Ukraine havitanuki bali vinamalizika kwa mazungumzo. 

Taarifa ya ofisi hiyo imesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona ni wajibu wake kuzuia kuenea vita vya Russia na Ukraine nje ya mipaka ya nchi hizo mbili na inaheshimu sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa.Mwanzoni mwa wiki iliyopita, shirika la habari la Reuters la utawala wa kifalme wa Uingereza lilidai kuwa Iran imeiuzia Russia idadi kubwa ya makombora mazito na yenye nguvu ya balestiki. Kwa mujibu wa madai ya shirika hilo la habari la utawala wa kifalme wa Uingereza, mkataba wa kijeshi baina ya Iran na Russia unachochea vikwazo zaidi vya Marekani. Chombo hicho cha habari cha Magharibi kimeeneza madai hayo ya uongo katika hali ambayo kwanza hakuna sheria yoyote inayozizuia Iran na Russia kuwa na mkataba wa kijeshi lakini zaidi ni kwamba, madola ya Magharibi yanaendelea kuisheheneza Ukraine aina kwa aina ya silaha za kushambulia Russia, lakini uungaji mkono huo wa nchi za Magharibi kwa Ukraine si kioja kwa mabanda hayo ya propaganda ya madola ya kibeberu kama Reuters ya Uingereza.

342/