Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, zaidi ya miezi minne imepita tangu nchi mbili za Iran na Sudan kutangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baina yao, hivi sasa Marekani na baadhi ya duru zinaingilia mara kwa mara uhusiano huo kwa visingizio mbalimbali.
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, John Godfrey, balozi wa Marekani nchini Sudan amesema katika mahojiano na waandishi wa habari kwamba: "Kuna ripoti za kuwa, kurejeshwa uhusiano kati ya Iran na Sudan kunaweza kujumuisha uungaji mkono wa kijeshi wa Iran kwa Sudan. Hili ni jambo linalotutia wasiwasi."
Amedai kuwa nchi za kigeni hazipaswi kuzipa silaha pande zinazopigana huko Sudan, wakati Marekani yenyewe ndiye muuzaji mkubwa wa silaha duniani ikiwemo kwa makundi hasimu nchini Sudan.
342/