Main Title

source : Parstoday
Jumapili

25 Februari 2024

17:22:55
1440268

Leo ni Nusu ya Shaaban, Siku ya Kuzaliwa Imam Mahdi AS

Leo Jumapili mwezi 15 Shaaban 1445 Hijria sawa na tarehe 25 Februari 2024 inasadifiana na kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam wa Zama hizi, Imam Mahdi AS na Imam wa 12 wa Waislamu wa Kishia.

Siku kama ya leo miaka 1190 iliyopita alizaliwa Imam Mahdi AS mwokozi wa ulimwengu katika mji wa Samarra, kaskazini mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq.

Yeye ni mwana mpendwa wa Imam Hassan Askari AS ambaye ni mmoja wa wajukuu wa Mtume Muhammad SAW. Miongoni mwa lakabu mashuhuri za Imam huyo wa Zama ni Mahdi, ambayo ina maana ya mtu aliyepewa hidaya na kuongozwa, na al Qaim, kwa maana ya atakayeanzisha mapambano.

Imam Mahdi AS alipitisha miaka mitano ya kwanza ya uhai wake akiwa chini ya malezi ya baba yake mpendwa, Imam Askari AS. Alichukua jukumu la kuongoza Umma wa Kiislamu kama Imam baada ya kuuawa shahidi baba yake mtukufu na kisha akatoweka na kwenda ghaiba kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu.

Kwa muda wa miaka 69 mtukufu huyo alikuwa akiwasiliana na kuwaongoza Waislamu kupitia wawakilishi wake maalumu. Baada ya hapo na kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Imam Mahdi AS alienda kwenye ghaiba kubwa na ya muda mrefu na atadhihiri tena ulimwenguni wakati mwafaka ambao Mwenyezi Mungu ataona unafaa.

Atakapodhihiri duniani, ataijaza ulimwengu kwa uadilifu na usawa baada ya kujaa dhulma na uonevu. Siku ya kuzaliwa mtukufu huyo huadhimishwa nchini Iran kama Siku ya Waliodhulumiwa Duniani. 

Tunatoa mkono wa kheri na baraka kwa wapenda haki wote na hasa wafuasi wa kweli wa Ahlul Bayti wa Bwana Mtume Muhammad SAW kwa mnasaba wa kuchomoza nuru hiyo ya haki.

342/