Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

26 Februari 2024

19:24:53
1440571

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Jaish al Dhulm aangamizwa katika hujuma ya askari usalama wa Iran

Kiongozi wa kundi la kigaidi la "Jaish al-Dhulm" ameuawa katika shambulio la askari usalama wa Iran.

Ismail Shah Bakhsh, mmoja kati ya viongozi wakuu wa kundi la kigaidi la "Jaish al-Dhulm" na mhusika mkuu wa mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi kusini mashariki mwa Iran, pamoja na wenzake kadhaa, wameangamizwa katika mapigano ya silaha na askari usalama wa Iran. 

Kundi hilo la kigaidi la Jaish al-Dhulm limehusika na mashambulizi kadhaa dhidi ya askari usalama na raia wasio na hatia wa mkoa wa Sistan na Baluchistan karibu na mpaka wa Pakistan, ikiwemo jinai ya kigaidi ya mwaka 2010 katika mkoa huo ulioko kusini mashariki mwa Iran.

Kundi hilo la kigaidi pia limehusika na mashambulizi mengine hapa nchini ikiwemo shambulizi dhidi ya waumini katika Msikiti wa Jamia na Msikiti wa Imam Ali (AS) huko Zahedan, mlipuko wa basi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwenye Barabara ya Khash, na hujuma ya kigaidi ya Chabahar mnamo 2011, ambayo iliua shahidi idadi kubwa ya watu katika Mkoa wa Sistan na Baluchistan.

Askari usalama wa Irani pia wamemkamata gaidi anayejulikana kama "Akram Lahori" katika mkoa wa Hormozgan, kusini mwa Iran.

Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, tawala za Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wao wa kikanda wamekuwa wakifanya harakati mbalimbali za kudhoofisha na kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu lakini njama hizo zote zimefeli na kushindwa.

342/