Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

26 Februari 2024

19:26:35
1440576

Russia yakosoa sera za kinafiki za Magharibi kuhusu hali ya Ukanda Gaza

Balozi na mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amekataa kusikiliza maneno ya wawakilishi wa nchi za Magharibi kuhusiana na suala la vita vya Ukraine na amekosoa vikali "unafiki na sera za kindumakuwili" za Magharibi kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Vassily Nebenzia ametangaza msimamo huo katika kikao cha Baraza la Usalama la Mataifa Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa kutimia miaka miwili ya vita baina ya Russia na Ukraine. Nebenzia amesema hasikilizi taarifa na matamshi ya wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na nchi za Magharibi katika kikako hicho.

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika mkutano huu wa Baraza la Usalama kwamba: "Ningependa kuonya mapema kwamba sitasikiliza tabano za wawakilishi wa Umoja wa Ulaya. Wacha waoneshane uwezo wao wa kuzungumza na kuchafua mkutano huu kwa kauli za kinafiki."Vassily Nebenzia amewaambia wawakilishi wa nchi za Magharibi kwamba: "Hakuna hata nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Magharibi kwa ujumla iliyowahi kupendekeza mpango wa kuitishwa kikao cha Baraza la Usalama walau mara moja kujadili mgogoro wa Gaza. Suala hili linaonesha zaidi unafiki na misimamo yenu ya kindumakuwili." Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, utawala ghasibu wa Israel, ukiungwa mkono na kusaidiwa kamilifu na nchi za Magharibi, umekuwa ukifanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina. Mauaji haya yanaendelea kufanyika chini ya kivuli cha kimya cha nchi za Maghariabi na taasisi zao eti za kutetea haki za binadamu. Wapalestina wasiopungua elfu 30 wameuawa hadi sasa wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo. 

342/