Main Title

source : Parstoday
Jumanne

27 Februari 2024

19:40:07
1440873

OIC yaziomba nchi zote duniani zisiuuzie silaha utawala wa Kizayuni wa Israel

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amezitaka nchi zote duniani kuacha kutuma silaha na zana za kijeshi kwa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel.

Hissein Brahim Taha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, amesema hayo katika kikao cha kuchunguza matokeo ya kisheria ya sera za uchokozi za Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi, na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano wa jamii ya kimataifa katika kusimamisha utumaji wa silaha kwa utawala wa Kizayuni.

Hissein Brahim Taha amelaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kuiambia jamii ya kimataifa kuwa: "Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina yanaambatana na hatari ya jinai za kivita na mauaji ya kimbari kwa kiwango kikubwa katika Ukanda wa Gaza."

Mwakilishi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu katika kikao kinachojadili masuala ya kisheria ya jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza, amesema yanayojiri sasa huko Palestina na ukiukaji wa haki za binadamu wa Israel vinapaswa kuwa katika ajenda ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu jana Jumatatu ilihitimisha wiki moja ya vikao vya kusikiliza mashauri ya kisheria ya uvamizi wa Israel na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina tangu mwaka 1967. Nchi 52 ziliitwa kutoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu na waliohudhuria katika vikao hivyo walitaka kukomeshwa uvamizi wa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina. Utawala haramu wa Israel haushiriki katika vikao hivyo, lakini tarehe 24 Julai 2023, ulituma barua kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu, ukiiomba mahakama hiyo ijizuie kutoa hukumu juu ya kesi ya jinai za kivita.

342/