Main Title

source : Parstoday
Jumanne

27 Februari 2024

19:54:53
1440879

Kubainishwa misimamo ya Iran kuhusu haki za binadamu katika Mkutano wa Geneva

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasilisha misimamo na mitazamo ya Iran kuhusu haki za binadamu katika mkutano wa 55 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian Jumatatu ya jana (Februari 26) aliwasili Geneva, Uswisi kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 55 wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amehutubia katika kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Haki za Binadamu na sehemu ya ngazi ya juu ya Kongamano la Upokonyaji Silaha la Umoja wa Mataifa. Sambamba na kushiriki katika kikao kidogo cha Palestina, Amir Abdollahian ameeleza misimamo na mitazamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Palestina na mgogoro unaoendelea Gazah na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani na serikali za Ulaya zimejaribu kujionyesha kama wafuasi wa haki za binadamu na zimetumia vyombo vya habari mashuhuri na vyenye mitazamo sawa na ya kwao ili kuonyesha sura ya kibinadamu.

Serikali za Magharibi, daima zimekkuwa zikilitumia suala la haki za binadamu kama wenzo wa malengo ya kisiasa na huzitambuliisha nchi huru ambazo haziko tayari kuburuzwa nazo kuwa ni maadui wa haki za binadamu. Matukio ya kisiasa ya ulimwengu katika miaka ya hivi karibuni yamefichua kwamba, haki za binadamu zinazopigiwa upatu na serikali za Magharibi zina vigezo vyake.Serikali za Magharibi zimenyamazia kimya mara chungu nzima mauaji makubwa ya halaiki hususan ya Waislamu katika sehemu mbalimbali za dunia, na hazikuwa tayari kulipa hata gharama ndogo kabisa  ya suala hili.

Mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Bosnia na Herzegovina na Myanmar ni miongoni mwa kesi ambazo wadai wa haki za binadamu wamenyamazia kimya na kuwa pamoja na watendaji wa jinai hizo na kuunga mkono vitendo vyao.

Mfano mwingine wa wazi ni ubaguzi na muamala na Waislamu katika nchi nyingi za Ulaya na Magharibi, ambapo serikali za Magharibi hata zinaweka mipaka ya ibada na mavazi ya Waislamu kwa kuweka sheria za upande mmoja.

Uungaji mkono wa viongozi wa nchi za Ulaya kwa vitendo vya kikatili vya makundi ya kibaguzi pamoja na mashambulizi ya nyama na mauaji ya Waislamu katika nchi hizi, ni mifano mingine ya ada hizi za kujikariri na za kibaguzi katika nchi za Magharibi.

Lakini jambo la kuzingatia katika kutoa tathmini na uchambuzi wa kwa nini sera na vitendo vya kibaguzi vya serikali za Magharibi ni ukimya wao kuhusiana na matusi na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na thamani za Kiislamu, na kwamba katika sheria za nchi hizo hakuna sheria hata ya kuwashtaki na kuwaadhibu watu waovunjia heshima matukufu ya wengine.