Main Title

source : Parstoday
Jumanne

27 Februari 2024

19:56:02
1440881

Amir-Abdollahian: Kuendelea vita Gazah kutazidi kuzorotesha hali ya kibinadamu

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel utazidisha hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo kwa kuendeleza vita katika Ukanda wa Gazah.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo mjini Geneva Uswisi katika mazungumzo yake na Mirjana Spoljarc Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Duniani na kuitaja hali ya kibinadamu ya Palestina kuwa tata na inatia wasiwasi sana. Abdollahian amesema pia kuwa, kwa bahati mbaya, utendaji ghalati na mbovu wa wa kisiasa umesababisha hadi sasa juhudi za kisiasa za kumaliza mzozo wa Gazah kutokuwa na natija maridhawa.

Akigusia matamshi ya baadhi ya nchi ikiwemo Marekani kuhusiana na Gazah ya baada ya vita na kuhusisha na kusitishwa kwa vita hivyo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa wa Iran amefafanua kwa kusema kuwa, viongozi wa makundi ya Palestina wanazingatia mbinu za kidemokrasia na makubaliano ya kisiasa kati ya Wapalestina wote na makundi ya Kipalestina na kuunga mkono njia hii ni kuunga mkono njia ya kidemokrasia.Amir-Abdollahian ameongeza kuwa: "Matukio katika Ukanda wa Gazah yanaonyesha wazi maafa ya kibinadamu, na vitisho vya utawala wa Israel vya kutaka kuishambulia Rafah vinaweza kuongeza ukubwa wa maafa hayo na kuwafanya Wapalestina milioni 1.4 waliokimbia makazi yao wanaoishi Rafah kukabiliwa na tishio kubwa. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran aidha amesisitiza kuendelezwa juhudi za kisiasa za Jamhuri ya Kiislamu ya kuhitimisha vita vya Ukanda wa Gazah.

342/