Kwa mujibu wa shirika la habari la Wanachuo wa Iran (ISNA), Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohammad Hassan Abu Turabi-Fard, ameeleza katika khutba za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran kwamba: kuinua kiwango cha ushiriki wa wasomi katika upitishaji maamuzi ya msingi, kurasimisha utawala wa sheria, kuwepo usimamizi wa wananchi juu ya madaraka, kupunguza kiwango cha uendeshaji mambo kupitia Serikali na kueneza utamaduni wa utoaji nafasi kwa wenye sifa kunapunguza mitafaruku na kuwafanya watu wawe wachangamfu katika masuala ya kijamii na huongeza kiwango cha motisha, matumaini na ushiriki wao katika mambo.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameeleza kuwa, umoja wa kitaifa na mshikamano wa Kiislamu ni stratijia na mikakati miwili isiyo na shaka ya kuimarisha mihimili ya mamlaka ya kitaifa na kugeuza vitisho kuwa fursa na akaongeza kuwa: taifa lenye umoja ni nembo ya azma, irada, matumaini na matarajio ya juu.
Abu Turabi-Fard ameendelea kubainisha kwamba: katika utawala uliotokana na matakwa ya wananchi na unaosimamia misingi ya sheria, mfungamano wa karibu na ulioshikamana wa raia katika uendeshaji wa nchi na uundaji wa taasisi na mifumo ya kisiasa ni miongoni mwa nguzo muhimu zaidi za demokrasia ya kidini na mamlaka ya kitaifa.../
342/