Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Machi 2024

09:41:19
1441607

Rais wa Cuba: Mauaji dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza ni Holocaust halisi

Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba amesema kuwa, mauaji yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza ni Holocaust halisi na ya kweli.

Rais Diaz-Canel amesema hayo katika video kwenye mtandao wa kijamii wa X na kubainisha kwamba, watu wa Cuba hawatapuuza uhalifu huu na watashiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Kuunga Mkono Watu wa Palestina Jumamosi.

Akigusia jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina, Rais wa Cuba amesisitiza kuwa, ukatili basi, unyanyasaji basi, kinga basi tena inatosha.

Aidha amesema kuwa Ukanda wa Gaza umegeuka kuwa kambi ya mauaji ya watu na gereza kubwa zaidi la wazi duniani kufuatia jinai na mashambulizi ya mfululizo ya Israel, na kusema kuwa jamii hii ya binadamu Gaza imekuwa ikishuhudia kutokea kwa mauaji mapya ya kutisha tangu miezi mitano iliyopita.