Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Machi 2024

09:44:17
1441612

Raisi awasili Algeria kushiriki Mkutano wa Saba wa Nchi za Gesi Duniani

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Algiers mji mkuu wa Algeria na kulakiwa katika uwanja wa ndege na Nadir Larbaoui, Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Saa chache zijazo Dkt Raisi atahutubia Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani (GECF) na pembezoni mwa mkutano huu atakutana na kuzungumza na baadhi ya viongozi na viongozi wa ngazi za juu wanaoshiriki katika mkutano huo.

Kufanyika hafla ya kukaribishwa rasmi na rais wa Algeria, mkutano na mazungumzo ya pande mbili na mwenzake wa Algeria, mkutano na wajumbe wa ngazi za juu wa nchi hizo mbili na kutiwa saini hati kadhaa za ushirikiano ni miongoni mwa ratiba ya siku ya pili ya safari ya Rais Ebrahim Raisi nchini Algeria. 

Akizungumza kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Algeria mapema jana Rais wa Iran alisema kwamba, bara la Afrika lina nafasi muhimu katika sera za kigeni za serikali ya Iran na kuongeza kuwa: "Uhusiano na Afrika kwa ujumla na hasa nchi za Kiislamu barani Afrika una nafasi maalum sana katika sera zetu za kigeni."

Kuhusu safari yake ya Algeria Ebrahim Raisi alisema, safari hii ni kwa mwaliko wa Rais wa Algeria ili kushiriki katika Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani (GECF). Aidha alisema: "Ni safari ya kwanza baada ya miaka 16 kufanyika katika kiwango cha rais wa nchi. Kwa mtazamo wa taifa letu, Algeria ni nchi iliyosimama dhidi ya wakoloni na watu wetu wana kumbukumbu nzuri sana za mapambano ya taifa la Algeria.