Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Machi 2024

09:45:26
1441614

Raisi: Afrika ina nafasi muhimu katika sera ya kigeni ya serikali

Rais Seyed Ebrahim Raisi wa Iran amesisitiza kuwa, bara la Afrika lina nafasi muhimu katika sera za kigeni za serikali ya Iran na kuongeza kuwa: "Uhusiano na Afrika kwa ujumla na hasa nchi za Kiislamu barani Afrika una nafasi maalum sana katika sera zetu za kigeni."

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Iran, IRNA, kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Algeria mapema Jumamosi, Rais wa Iran amesema kwamba kwanza tunapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kushiriki kwa wingi wananchi kwenye vituo vya kupigia kura na akasema: "Lazima niwashukuru wananchi kwa uwajibikaji wao."

Kuhusu safari yake ya Algeria amesema kuwa safari hii ni kwa mwaliko wa Rais wa Algeria ili kushiriki katika Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani (GECF). Aidha amesema: "Ni safari ya kwanza baada ya miaka 16 kufanyika katika kiwango cha rais wa nchi. Kwa mtazamo wa taifa letu, Algeria ni nchi iliyosimama dhidi ya wakoloni na watu wetu wana kumbukumbu nzuri sana za mapambano ya taifa la Algeria.

Raisi ameitaja nafasi ya Algeria barani Afrika kuwa ni ya kipekee na kuongeza kuwa nchi hii iko katika nafasi muhimu ya ustaarabu wa Kiislamu na uhusiano wa Iran na Algeria unasaidia sana katika uhusiano wetu na Afrika. Aidha amesema nafasi ya Iran na Algeria katika Jumuiya ya Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani na katika ulimwengu wa Kiislamu ni nukta mbazo zimezileta nchi hizi mbili karibu zaidi.

Rais wa Iran amsema nukta nyingine ya pamoja baina ya nchi mbili ni mapambano dhidi ya sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja katika uga wa kimataifa.

Rais wa Iran akiashiria misimamo ya pamoja ya nchi mbili katika kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na hasa Gaza amesema: "Bila shaka katika kikao cha pande mbili tutajadili suala la Palestina ambalo hivi sasa si tu kuwa ni suala la ulimwengu wa Kiislamu bali pia ni suala la ubinadamu.