Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Machi 2024

19:57:54
1442206

Papa Francis atoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja huko Gaza

Kiongozi wa Wakatoliki duniani ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Papa Francis aliyekuwa akizungumza katika sala yake ya kila wiki, ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza, akisisitiza udharura wa kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel na kuongezwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza.Hapo awali, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Jassem Al-Badawi, na wawakilishi wa Morocco, Jordan na Misri, wamesisitiza mshikamano wao na taifa la Palestina, na kwa mara nyingine wametoa wito wa kusitishwa mapigano Ukanda wa Gaza na kutumwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa eneo hilo lilnaloendelea kushambuliwa na jeshi la utawala haramu wa Israel.

Sambamba na hayo, Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, pia ameyataja mazingira ya Ukanda wa Gaza kuwa si ya kibinadanuu na kusisitiza udharura wa kusitishwa vita mara moja katika eneo hilo. Makamu wa Rais wa Marekani ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kutayarisha mazingira yanayohitajika ili misaada zaidi iingizwe katika eneo hilo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa taarifa likielezea wasiwasi wake juu ya kuendelea mashambulizi ya Israel yanayolenga mikusanyiko ya raia wa Palestina katika eneo la kusambaza misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Baraza hilo pia limetoa wito wa kuzidishwa misaada ya kibindamu kwa watu wa Gaza, kulindwa raia wa Palestina na miundombinu ya Ukanda wa Gaza.Utawala pandikizi wa Israel ambao unasaidiwa kikamilifu na madola ya kibeberu hasa Marekani, unaendelea kupuuza amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina wa Ukanda wa Gaza na hadi sasa imeshaua shahidi zaidi ya Wapalestina 30,000 Oktoba mwaka jana na kujeruhi wengine karibu elfu 70, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.

342/