Main Title

source : Parstoday
Jumanne

5 Machi 2024

18:55:15
1442452

Kiongozi Muadhamu: Kushiriki katika uchaguzi ilikuwa jihadi ya watu wa Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru mahudhurioa ya taifa la Iran katika vituo vya kupigia kura Machi Mosi na kusema: "Kushiriki taifa la Iran katika uchaguzi huo lilikuwa jukumu la kijamii, kiustaarabu na kijihadi."

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ​​(Jumanne) baada ya kupanda miche mitatu kwa mnasaba wa Siku ya Upandaji Miti Iran ameongeza kuwa: "Maadui walijaribu kwa takriban mwaka mmoja kueneza propaganda za kuwazuwia watu wasishiriki katika chaguzi ili kusiwe na ustawi lakini wameshindwa. Hata hivyo kwa hamasa yao kubwa na ya ajabu ya Machi, wananchi walijitokeza kukabiliana na njama za maadui, hivyo harakati hii ilikuwa jihadi."

Ayatullah Khamenei pia amewashukuru walioshiriki katika uchaguzi huo, wakiwemo waliohusika katika kuandaa, kutangaza na kudumisha usalama.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia mafuriko katika maeneo ya kusini mwa mkoa wa Sistan na Baluchistan, kusini-mashariki mwa Iran, na hasara waliyopata wananchi na kusisitiza kuhusu ulazima wa kuendeleza kutolewa misaada inayotolewa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali. Aidha amesema wenye uwezo wa kuingiza misaada na kusaidia wapeleke misaada katika eneo hilo.Ayatullah Khamenei aidha ameashiria Siku ya Upandaji Miti Iran na kutaja upandaji miti kuwa ni uwekezaji wa gharama nafuu na wenye faida na kuongeza kuwa: "Mti una matunda mengi kama vile kuongeza hewa ya oksijeni na kupambana na uchafuzi wa mazingira, hivyo ni uwekezaji wenye faida hasa katika maisha ya kimashine ya leo." Aidha amesema, kwa bahati mbaya, uchafuzi umeongezeka.

Aidha ameashiria kuhusu namna Uislamu unavyolipatia umuhimu suala la uhusiano kati ya mwanadamu na mazingira na pia utunzaji wa mazingira, ambapo amepanda miche mitatu ukiwemo mzeituni ili kuonyesha umakini zaidi katika upandaji miti na kuongeza kuwa: "Katika kutangaza mshikamano na huruma kwa watu waliodhulumiwa wa Palestina wenye uwezo mkubwa wa mapambano, moja ya miche iliyopandwa leo ni mzeituni na kitendo hiki cha kinembo ni kuwatumia salamu Wapalestina."

Mbali na kupanda mzeituni, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amepanda mche mmoja wa mteashuri na mwingine wa mtini ambao ulizalishwa nchini.
Mtini ni mti wa asili wa misitu ya Mazandaran, ambao pamoja na kutumika mbao zake ngumu kwa malengo mbalimbali, mizizi na majani yake pia hutumika kwa ajili ya dawa.
Nchini Iran, Machi 5 hadi 12 inaitwa "Wiki ya Maliasili" ambapo siku ya kwanza ya wiki hii (Machi 5) ni siku ya upandaji miti.