Main Title

source : Parstoday
Jumanne

5 Machi 2024

18:55:45
1442453

Iran: OIC inakabiliwa na 'mtihani mgumu' kuhusu uhalifu wa Israel, himaya ya Marekani kwa utawala huo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza umuhimu wa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) unaotarajiwa kufanyika leo, akisema jumuiya hiyo yenye wanachama 57 "inakabiliwa na mtihani" juu ya vita vya mauaji ya kimbari vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Nasser Kan’ani aliyasema hayo jana Jumatatu katika kikao chake cha kila wiki na waandishi wa habari, siku moja kabla ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC kuhusu vita vya Gaza, kinachofanyika leo katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia. 

"Vita hivi vya kikatili vinaendelea katika kivuli cha uchochezi wa maofisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel na uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani. OIC inakabiliwa na mtihani hii leo kuonesha itatumia vipi uwezo wake kuitetea Palestina,” alisema.

Kan'ani amesema: "Viongozi wa nchi za Kiislamu wanatarajiwa kuchukua uamuzi madhubuti na wa pamoja unaohitaji hatua madhubuti ya kuilinda Palestina, na udharura ya kusimamisha vita."

Hadi sasa utawala katili wa Israel umeuwa Wapalestina wasiopungua 30,534 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 71,920.

342/