Main Title

source : Parstoday
Jumanne

5 Machi 2024

18:57:13
1442456

Ebrahim Raisi: Usalama wa Iran hautegemei nchi yoyote

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, usalama wa taifa la Iran hautegemei nchi yoyote ile.

Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika hafla ya mahafali ya Chuo Kikuu cha Polisi na kueleza kwamba usalama wa taifa la Iran ya leo unatokana na mahudhurio ya watu katika nyanja na medani tofauti na kutokana na mwamko, uelewa, weledi, umakini na kuwa macho vikosi vya jeshi na polisi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaja mambo kama uzoefu, ujasiri, ujuzi, ushujaa, imani kwa Mwenyezi Mungu, kupenda mapinduzi ya Kiislamu na upendo kwa watu, na uwepo endelevu katika kutoa huduma kuwa ni sifa kuu za kikosi cha polisi cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Aidha Ebrahim Raisi amesema katika mahafali hayo kwamba, vikosi na majeshi ni chimbuko la fakhari ya taifa na yana nafasi muhimu katika moyo wa taifa kwa sababu daima yapo pamoja na watu.

Kadhalika Raisi sambamba na kubainisha kwamba, adui pamoja na uadui wake wote alioufanya dhidi ya taifa la Iran anajua kwamba, leo wananchi ndio sehemu muhimu zaidi ya uwezo na mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kwamba, mipango yote ya adui imeshindwa na kugonga mwamba katika kipindii chote hiki cha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

342/