Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

7 Machi 2024

14:15:41
1442840

Iran yatwaa meli ya mafuta ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanikiwa kukamata meli ya kubebea mafuta ya Marekani katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

Shirika la habari la Mehr limetangaza habari hiyo leo Jumatano na kuongeza kuwa, kunaswa kwa meli hiyo ya mizigo ya Marekani yenye jina la 'Advantage Sweet' kumejiri kutokana na amri ya mahakama ya Iran.

Mahakama moja ya Tehran ilitoa amri ya kukamatwa kwa meli hiyo ya Marekani baada ya Wairani wanaogua maradhi ya ngozi ya Epidermolysis Bullosa (EB) kuwasilisha malalamishi dhidi ya Washington.

Wagonjwa hao waliiambia mahakama hiyo ya uhusiano wa kimataifa (tawi la 55) hapa Tehran kuwa, vikwazo vya kidhalimu na vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran vimezuia uingizwaji wa dawa wanazohitaji, na hivyo kukitaka chombo hicho cha sheria kitoa agizo la kuwajibishwa Washington.

Kutokana na vikwazo vya kikatili vya US dhidi ya Iran, kampuni ya Sweden ilikataa kuiuzia Iran bendeji maalumu za Mepilex na bidhaa nyingine za tiba zinazohitajiwa na wagonjwa wa EB. Ukosefu wa bendeji mbadala zinazofaa umepelekea watoto kadhaa wanaosumbuliwa na maradhi hayo hapa Iran kupoteza maisha yao.Januari mwaka huu pia, Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilitangaza kukamata meli nyingine ya mafuta ya Marekani kwa amri ya mahakama katika Bahari ya Oman. Tehran ilisema kukamatwa meli ya Suez Rajan, Mei mwaka jana, na wizi wa mafuta ya Iran uliofanywa na Marekani kwenye meli hiyo, kulitokana na kukamatawa meli ya mafuta ya US yenye jina jipya St Nicholas katika maji ya Bahari ya Oman.

Si vibaya kuashiria hapa kuwa, Marekani imekuwa ikitumia mabavu kutwaa meli zinazopakia mafuta za Iran na nchi nyingine katika maji ya kimataifa na kuiba bidhaa hiyo.