"Tunaunga mkono Palestina kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa," amesema Wang Yi katika mkutano na waandishi wa habari. Wang amebainisha kuwa, maafa ya Ghaza kwa mara nyingine tena yameukumbusha ulimwengu kwamba ukweli kuwa maeneo ya Palestina yamekaliwa kwa mabavu kwa muda mrefu hauwezi tena kupuuzwa. Ameongeza kuwa, takwa la muda mrefu la watu wa Palestina la kuanzisha nchi huru haliwezi kuepukika tena, na dhulma ya kihistoria wanayopata watu wa Palestina haiwezi kuendelea kwa vizazi bila ya kurekebishwa.Beijing imekuwa ikitoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano tangu utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vya sasa vya kikatili na mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Ghaza Oktoba 7 mwaka jana.
source : Parstoday
Alhamisi
7 Machi 2024
14:16:11
1442841
Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema nchi yake inaunga mkono Palestina kupewa uanachama "kamili" wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa takwa la muda mrefu la watu wa Palestina la kuanzisha nchi yao huru haliwezi kuepukika tena.