Yamamoto, mwanachama wa Taasisi ya Taaluma za Kituruki ya Chuo Kikuu cha Marmara ameeleza kwamba, kumekuwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na Wapalestina katika nchi yake kufuatia mashambulio ya Oktoba 7, 2023. Mwanaakademia huyo amebainisha kuwa, kauli za chuki dhidi ya Waislamu zimeongezeka nchini Japan kutokana na kuongezeka uungaji mkono kwa vyama vya mrengo wa kulia. Yamamoto amesisitiza kwamba chuki dhidi ya wageni (xenophobia), ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi katika nchi hiyo ya Asia Mashariki, zimegeuka kuwa chuki dhidi ya Waislamu baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza.Ameendelea kueleza kwamba hivi sasa Japan inashuhudia mabadiliko hasi ambapo chuki dhidi ya wageni na chuki dhidi ya Waislamu zimeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.