Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Machi 2024

19:45:28
1443261

Wapalestina watano wauawa na misaada wa kudondoshwa kutoka angani, Gaza

Wapalestina watano wameuawa na vifurushi vya misaada vilivyodondoshwa na ndege za Marekani na washirika wake kwenye Ukanda wa Gaza unaozingirwa na Israel, huku mamlaka ya Gaza ikilishutumu zoezi hilo kuwa ni "propaganda tupu" na sio huduma ya kibinadamu.

Msemaji wa Kikosi cha Ulinzi wa Raia huko Gaza, Mahmoud Basal, amesema maboksi yaliyodondoshwa na Marekani na washitrika wake yaliangukia juu ya watu waliokata tamaa waliokuwa wamekusanyika kaskazini-magharibi mwa Jiji la Gaza siku ya Ijumaa ili kukusanya misaada hiyo, baada ya ndege za kiraia kudondosha misaada maeneo ya mbali kimakosa.

Ripoti zinasema, makosa ya kiufundi katika zoezi hilo yamepelekewa kujeruhiwa idadi isiyojulikana ya watu wa Gaza.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha ndege ikidondosha vifurushi vya msaada kwa watu katika Kambi ya al-Shati kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Wenyeji wanasema miavuli iliyotumika kudondosha misaada haikufunguka, na kusababisha masanduku kuwaangukia watu wanaohitaji sana msaada ya chakula, maji na dawa.Madakraei katika Hospitali ya Al-Shifa Medical Complex wanasema, baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya. Ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ya Gaza imesema operesheni kama hizo ni "batili" na "sio njia bora ya kuwasilisha msaada kwa waathiriwa wa mshambulizi ya Israel.

342/