Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Machi 2024

19:46:49
1443263

Jeshi la Yemen lashambulia meli na manuwari za kivita za Marekani, Ghuba ya Aden

Msemaji wa jeshi la Yemen, Yahya Saree amesema kuwa kundi hilo limefanya operesheni za aina yake ambazo zimelenga meli ya Marekani katika Ghuba ya Aden kwa kutumia makombora kadhaa, na manuari za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden kwa kutumia ndege 37 zisizo na rubani.

Saree amesema oparesheni hizo mbili zilifanikiwa kufikia malengo waliyoyatarajia na kusisitiza kuwa, kundi hilo litaendeleza operesheni zake katika eneo la Bahari Nyekundu hadi pale hujuma dhidi ya Ukanda wa Gaza zitakapokoma na mzingiro wa eneo hilo kuondolewawa.Wakati huo huo Marekani imekiri kwamba wapiganaji wa Yemen wamerusha makombora mawili ya balestiki dhidi ya meli ya "MV Propel Fortune" katika Ghuba ya Aden na kufanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani. Hata hivyo uongozi wa jeshi la Marekani umedai kuwa umetungua ndege nyingi za wapiganaji wa Yemen. Alhamisi iliyopita taasisi ya kigaidi ya CENTCOM ya Marekani ilithibitisha kwamba watu 3 wameuawa na wengine 4 wamejeruhiwa katika shambulio la jeshi la Yemeni dhidi ya meli ya Marekani katika Bahari Nyekundu au Bahari ya Sham. Sambamba na kushadidi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, wanajeshi wa Yemen wameamua kuzuia meli zote zinazohusiana na utawala huo katili na zile zilizoko safarini kuelekea Israel. Operesheni hizo zimewasababishia hasara kubwa Wazayuni na ndio maana madola ya kibeberu ya Marekani na Uingereza yameanzisha vita dhidi ya Yemen ili kuunga mkono jinai za Israel huko Gaza.

342/