Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Machi 2024

19:47:55
1443265

Kuhani wa Kiyahudi ahamasisha Wazayuni wafanye mauaji ya kimbari Ghaza

Kuhani mwanamgambo na mhubiri wa mahubiri ya Kizayuni ya utoaji vitisho, Eliyahu Mali, ametoa wito wa kufanywa mauaji ya kimbari ya Wapalestina waliowekewa mzingiro huko Ghaza, akidai kuwa kufanya hivyo kunaendana na Halakha, yaani sheria ya Kiyahudi.

Mahubiri hayo ya utoaji vitisho yanatolewa wakati utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza mauaji ya kimbari huko Ghaza bila kujali maandamano ya upinzani yanayofanyika kote duniani na miito ya kuutaka uondoe wanajeshi wake katika eneo hilo.Mali, ambaye anaongoza skuli ya kidini ya Shirat Moshe yenye itikadi na misimamo mikali ndani ya jamii ya Kizayuni, ambayo wanafunzi wake wanahudumu katika jeshi, amesema "hakuna watu wasio na hatia" huko Ghaza; na watoto wote wachanga katika eneo hilo dogo lazima wachinjwe. Katika mkanda wa video uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kuhani huyo anaonekana akiihutubu hadhira: "katika vita vyetu vya mitzvah [vitakatifu], katika hali yetu ya Ghaza, kulingana na sheria inavyosema, 'si kila nafsi itaishi,' na mantiki ya hili ni wazi sana: ikiwa hutawaua, watakuua wewe". Mali amedai kwamba wale waliotajwa kuwa ni "waharibifu" katika vita vya leo ni "watoto wa vita vya awali ambao tuliwaweka hai, na kwa hakika, ni wanawake ndio wanaozalisha magaidi"; na akaendelea kusema: “leo ni mtoto mchanga, kesho ni mpiganaji”.Kuhani huyo wa Kizayuni ameendelea kusema: "yeyote anayekuja kukuua kwa dhana hii haijumuishi tu kijana wa miaka 16, 18, 20, au 30 ambaye sasa anakunyooshea silaha, lakini pia kizazi kijacho cha [wana wa Ghaza], na wale wanaozaa kizazi kijacho [ yaani wanawake wa Ghaza], kwa sababu kiukweli hakuna tofauti". Kauli hizo za kiuadui na kigaidi za kiongozi huyo wa kidini wa Kizayuni zinatolewa wakati utawala haramu wa Israel ukiwa tayari umeshaua zaidi ya Wapalestina 30,800 na kujeruhi karibu 73,000 katika vita vyake vya kikatili na vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza. Israel imeshtakiwa na inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliotolewa na mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa uliiamuru Tel Aviv isitishe vitendo vya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua za kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa na kuwafikia raia Wapalestina walioko Ghaza.../