Kazem Gharibabadi, Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran ameyasema hayo katika barua tatu zinazofanana kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu kwa munasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake siku ya Ijumaa.
Akizungumzia uhalifu wa Israel huko Gaza, Gharibabadi amesema "kinachosikitisha zaidi... ni hali ya wanawake na wasichana."
Amebainisha kuwa wanawake na watoto ni asilimia 70 ya waliouawa au kujeruhiwa katika vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Katika barua zake, Gharibabadi amerejelea ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa zilizofichua athari mbaya ya vita kwa wanawake na wasichana wa Gaza.
342/