Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

11 Machi 2024

14:45:54
1443708

Iran yasambaratisha mtandao wa Uingereza wa uhalifu wa kifedha na kamari ya intaneti

Wizara ya Usalama ya Iran imefanikiwa kusambaratisha mtandao mkubwa wa kamari au kubeti kwa njia ya intaneti ambao ulikuwa unaendeshwa na watu wahalifu wakiwa Uingereza.

Wizara hiyo ilitoa tangazo hilo katika taarifa Jumamosi, ikisema mafanikio hayo yamepatukana kufuatia miezi 14 ya "upelelezi mgumu."

Mtandao huo ulikuwa umefaulu kulaghai pesa nyingi, kwa kutumia akaunti za benki zipatazo 35,006, njia 1,200 za malipo, na tovuti 54 kubwa za kamari au kubeti.

Taarifa hiyo imesema: "Mtandao wa mafia wenye makao yake London" uliweka sehemu ya pesa ambazo zilipokewa kutoka kwa wacheza kamari hadi kwenye akaunti na kisha kuhamisha kiasi kikubwa cha pesa zao hadi Uingereza.

Wizara hiyo imebainisha kuwa serikali ya Uingereza imekuwa ikifumbia macho utakatishaji wa fedha haramu katika mtandao wa mafia na shughuli nyingine haramu kwa kisingizio kuwa wahalaifu hao ni walipa ushuru mkubwa kwa faida yao. Kwa msingi huo serikali ya Uingereza kimsingi "ilifungua njia kwa wahalifu wa uhalifu," ilisema katika taarifa hiyo.

Maafisa wa wizara ya usalama ya Iran pia waliwakamata mameneja watano wanaoendesha mtandao wa "Nitro bet" na mfumo wa malipo wa  "Pardakht.me" kwa tuhuma za kuhujumu uchumi, kuendesha tovti za kamari, na kupata faida kupitia njia haramu.

Shughuli za mtandao huo wenye makao yake makuu nchini Uingereza hazikuishia kwenye ulaghai tu, ilisema wizara hiyo, na kuongeza kuwa, wakati huo huo, ilikuwa ni kutafuta uhalalishaji kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kucheza kamari.

342/