Main Title

source : Parstoday
Jumanne

12 Machi 2024

19:40:47
1443993

Hizbullah yajibu mashambulizi kwa kuupiga utawala wa Kizayuni kwa makombora 100

Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon mapema leo Jumanne, umekipiga kwa makombora zaidi ya 100 ya Katyusha, kituo kikuu cha ulinzi wa anga cha utawala wa Kizayuni katika maeneo ya kaskazini mwa Palestina yaliyopachikwa jinai bandia la Israel.

Hayo yameripotiwa na mwandishi wa televisheni ya al Alam aliyeko kusini mwa Lebanon ambaye ameripoti kuwa, shambulio hilo la makumi ya makombora dhidi ya kambi ya kijeshi ya Israel limefanywa na harakati ya Hizbullah ili kujibu shambulizi la Israel lililofanyika jana usiku mashariki mwa Lebanon.

Mwandishi huo amesema kuwa, majibu hayo makali ya muqawama wa Kiislamu wa Lebanon yametolewa haraka sana na bila ya kumpa nafasi adui ya kufikiria kilichotokea. 

Katika upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, harakati hiyo inafanya mashambulizi yake dhidi ya Wazayuni kwa mujibu wa mashambulio ya utawala wa Kizayuni na kwamba uungaji mkono wa kivitendo wa Hizbullah kwa wananchi wa Ghaza, utaendelea.Sheikh Naim Qassim amesema hayo na kuongeza kuwa wanamapambano wa Hizbullah wamejiandaa kukamilifu kupambana na mashambulizi ya Israel kwa hali yoyote na kwa ukubwa wowote. Amesema: Maadamu uvamizi wa Israel huko Ghaza unaendelea, Hizbullah nayo itaendelea kuushambulia utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono kivitendo watu wa Ghaza. Huku hayo yakiripotiwa, Yair Lapid, kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid ndani ya utawala wa Kizayuni amekiri kushadidi hitilafu na mizozo baina ya vyama vya upinzani na Baraza la Mawaziri la utawala la Israel. Yair Lapid, amesema kuwa, Benjamin Netanyahu, waziri wkuu wa utawala wa Kizayuni amepoteza imani ya nusu ya Baraza la Mawaziri na Wazayuni walio wengi. Matamshi ya Lapid ambaye chama chake kinahesabiwa kuwa kikubwa zaidi kinacholipinga Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni katika Bunge la Israel (Knesset) ni kiashirio cha wazi cha kushadidi ugomvi kati ya Netanyahu na vyama vya upinzani. Lapid anachukuliwa kuwa mpinzani mkuu wa Netanyahu.